×

Ebitoke Amlipua Nai Kisa ‘Do You Love Me’

Anastazia Exavery ‘Ebitoke’

MSANII wa vichekesho nchini,ambaye pia ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Anastazia Exavery ‘Ebitoke’ kwa mara ya kwanza ameropoka siri ya msanii mwenzake Nairath Ramadhani kuwa hana mbele wala nyuma.

 

Ebitokeo ametoa kauli hiyo baada ya Nai kudaiwa kumkosoa hadharani msanii huyo kuwa hajui kuimba na kutolea mfano wimbo wake alioutoa wa ‘Do you love me’.


Aidha, akizungumza na AMANI, Ebitoke alisema huwa anamshangaa sana Nai kwa kuwa ni mtu ambaye anapenda kuwasema wenzake vibaya.

“Ukimuangalia Nai hana cha maana mjini zaidi ya maisha ya kungaunga na kupanda bajaji.“Kila siku anapenda kusema kwamba wasichana sisi hatupendani … mimi nifanya kazi yangu, alafu anakuja mtu tu hajulikani alipotoka ananiambia nyimbo mbaya.“

 

Unajua nilimuangalia nikamshusha juu mpaka chini, angekuwa na cha maana hapa mjini ningesema niheshimu kauli yake niongeze juhudi,“ alisema Ebitoke.

 

NANDY: Sipendi Billnass awe karibu na wanawakeStori:Khadija BakariSexlady kunako anga la muziki mtamu wa Bongo Fleva, Faustina Charles ’Nandy” amefunguka kuwa kitu ambacho kitamfanya agombane na mpenzi wake ni kuwa na mazoea na wanawake.

 

Akipiga storing na AMANI, Nandy ambaye kwa sasa yupo kwenye uhusiano na msanii mwenzake, William Lyimo ’Billnass’, amesema hakuna mwanamke ambaye anapenda mpenzi wake awe karibu na wanawake wengine.

 

“Sipendi wala sitaki kuona mpenzi wangu akiwa karibu na wanawake, labda iwe kikazi tu na si vinginevyo.“Kwa sababu wanawake wanatabia ya kushawishi wanaume za watu, kwa hiyo sipendi mwanaume wangu awe karibu na wanawake kabisa tutagombana,” alisema Nandy.

Stori: Khadija Bakari

MBUNGE MWANA FA Apokea HUNDI ya MALIPO ya BIMA za WATOTO 100 Kutoka kwa MAUA SAMA…

Leave a Comment