×

Simba, Yanga Washindana Zawadi ya Spoti Xtra

Balozi wa Kampuni ya Vunjabei Mobile Shop, Blandina Chagula ‘Johari’, akimkabidhi Khalifa Rajab, zawadi ya jiko la gesi baada ya kuibuka mshindi wa Chemsha Bongo ya Spoti Xtra.

BAADA ya wiki iliyopita kushuhudia shabiki wa Simba, Peter Tarimo na wa Yanga, Fatuma Juma, wakifanikiwa kuibuka na zawadi kupitia Chemsha Bongo inayoendeshwa na Gazeti la Spoti Xtra, wiki hii pia mashabiki wengine wa Simba na Yanga wameibuka na zawadi.

 

Washindi wa wiki hii ni Albert Wilson mkazi wa Mwembeyanga ambaye ni shabiki wa Simba na Khalifa Rajab, mkazi wa Chanika anayeishabiki Yanga. Wawili hao wamejishindia zawadi kupitia Gazeti la Spoti Xtra, toleo la Desemba 6, mwaka huu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya seti ya vyombo katika ofisi za gazeti hili zilizopo Sinza Mori, Dar, leo Jumamosi, Wilson alisema: “Kama mdau mkubwa wa Spoti Xtra, nashukuru kwa zawadi hii, mimi ni shabiki wa Simba na mdau mkubwa wa michezo.

Washindi wa Chemsha Bongo ya Spoti Xtra, Khalifa Rajab (kushoto) na Albert Wilson, wakionyesha magazeti ya Spoti Xtra yaliyowapa ushindi.

“Nawashauri wapenda soka kununua magazeti haya na kushiriki Chemsha Bongo kwani kwa shilingi 500 tu unaweza kujishindia zawadi mbalimbali.”

 

Naye Rajab aliyejishindia jiko la gesi, alisema: “Kwa kweli mimi ni mdau mkubwa wa michezo na nimekuwa nikihakikisha napata mapema sana nakala yangu ya Gazeti la Spoti Xtra kutokana na namna lilivyosheheni habari za kutosha za michezo za ndani na nje ya Tanzania.

 

“Kama shabiki wa Yanga najivunia kupata taarifa za maendeleo ya timu yangu kupitia Spoti Xtra, huku nikijishindia zawadi mbalimbali, hivyo nawashauri wapenda soka wenzangu washiriki kwa kununua magazeti ya Spoti Xtra,” alisema.

Washindi wa Chemsha Bongo ya Spoti Xtra, Albert Wilson (kulia) na Khalifa Rajab, wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kampuni ya Vunjabei Mobile Shop, Blandina Chagula ‘Johari’ baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

Kwa upande wa Balozi wa Kampuni ya Vunjabei Mobile Shop ambao ndiyo wadhamini wa Chemsha Bongo hiyo, Blandina Chagula ‘Johari’, alisema: “Hii ni fursa kubwa kwa wadau wa soka kuhakikisha wanajishindia zawadi mbalimbali za majumbani kwa kitendo cha kununua Gazeti la Spoti Xtra.

 

“Lakini pia tunawakaribisha wateja wetu kupata bidhaa mbalimbali za majumbani kupitia maduka yetu ya Vunjabei Mobile Shop, tuna bidhaa bora na za uhakika.”

 

Mhariri wa Spoti Xtra, Omary Mdose, naye alisema: “Kama mnavyojua kuwa Gazeti la Spoti Xtra ndilo linaloongoza hapa nchini kwa ufanisi wa habari zinazoandikwa pamoja na uhakika wa takwimu.

 

“Hivyo usipange kukosa nakala yako, kwani kwa kufanya hivyo unajiweka katika nafasi nzuri ya kushinda zawadi kutoka kwa washirika wetu Kampuni ya Vunjabei Mobile Shop.

Albert Wilson, akikabidhiwa zawadi yake ya vyombo na Balozi wa Kampuni ya Vunjabei Mobile Shop, Blandina Chagula ‘Johari’,  mara baada ya kuibuka mshindi wa Chemsha Bongo ya Spoti Xtra.

“Hii ni wiki ya pili tunatoa zawadi, wiki ijayo inaweza kuwa zamu yako, hivyo tunakusihi wewe msomaji wetu kununua Spoti Xtra na kushiriki Chemsha Bongo inayopatikana ukurasa wa pili ikiwa na maelekezo yote ya kushiriki.”

 

Spoti Xtra kwa kushirikiana na Vunjabei Mobile Shop, imeanzisha Chemsha Bongo hiyo ambayo lengo kubwa ni kuwaleta karibu wasomaji wake, huku pia ikiwa ni ujio wa Spoti Xtra Jumanne.

 

Kwa sasa Gazeti la Spoti Xtra linatoka mara tatu kwa wiki, JUMANNE, ALHAMISI na JUMAPILI kwa bei ileile ya Sh 500 tu.

Leave a Comment