×

Shigongo Akomaa na Daraja Korofi Buchosa

MBUNGE  wa Jimbo la Buchosa, Mh. Eric Shigongo amekagua ujenzi wa daraja la Mizolozolo barabara ya Sengerema – Nyehunge ambapo ameshirikiana na mafundi hao ili kuharakisha zaidi kukamilika mapema kwa ujenzi wa daraja hilo kabla ya mvua kubwa hazijaanza kunyesha.

 

Shigongo ambaye pia hata jana alifika katika ujenzi huo, amesema jambo kubwa analolifanya kwa hivi sasa ni kuhakikisha anashughulikia na kumaliza kero za wananchi ikiwemo miundombinu ya barabara kwa kutengeneza sehemu korofi katika barabara za jimbo hilo.

 

Pia kuna ujenzi wa madaraja pamoja na karavati ili kusaidia wananchi kupita kwa urahisi kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali zinazowapa kipato cha kila siku.

 

“Tunaendelea kufanya kazi za wananchi wetu ambao walitupa nafasi ya kuwatumikia katika kipindi cha miaka mitan.  Nimeamua kutengeneza barabara, madaraja na makalavati ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wetu; ninafahamu bado tuna kazi kubwa, lakini kwa ushirikiano wa pamoja tutazitatua kero hizi,” amesema Shigongo.

 

Leave a Comment