×

Bodi Ya Filamu Ilivyomkabidhi Bendera Muigizaji Aliyeshinda Tuzo ya Kimataifa

Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Kilonzo Kiango akizungumza kwenye hafla hiyo. Kulia ni muigizaji huyo Shaykaa.

BODI ya Filamu nchini, leo imemkabidhi bendera ya taifa muigizaji wa filamu za Kibongo, Shahista Alidina maarufu Shaykaa baada ya kushinda tuzo ya Muigizaji bora kupitia filamu ya Uhuru na gharama zake.

Akizungumza na wanahabari wakati akimkabidhi bendera hiyo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt. Kiango Kilonzo amesema Shaykaa anatarajiwa kukabidhiwa tuzo hiyo ya kimataifa ijulikanayo kama World Oscars Signature Award, Desemba 18 mwaka huko, Dubai U.A.E.

Shaykaa akiishuru Bodi ya Filamu nchini kwa kuutambua na kuheshimu ushindi wake na kuwashukuru wadau mbalimbali waliomsaidia kufanikisha kutwaa tuzo hiyo wakiwemo waandaaji wake Pilipili Entertainment.

Dkt. Kilonzo amesema Shaykaa ameipa sifa kubwa nchi yetu pamoja na tasnia ya filamu kwa kitendo cha filamu hiyo kuweza kupenya katika anga za kimataifa na kufikia kushinda tuzo hiyo yenye heshima kubwa ulimwenguni.

Baada ya Dkt. Kilonzo kumkabidhi Shaykaa bendera ya taifa amewasisitiza wasanii wengine kuboresha kazi zao ili nazo zionekanae kimataifa na kuizidishia sifa nchi yetu.

Mkurugenzi wa Pilipili Entertainment, Nilesh Batt ambaye kampuni yake ndiyo iliyoandaa filamu ya Uhuru na Gharamna zake iliyompa ushindi Shaykaa akizungumza kwenye hafla hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Pilipili Entertainment ambao ndiyo waliyoiandaa filamu hiyo, Nilesh Batt amesema Shaykaa alistaili kupewa tuzo hiyo kutokana na jinsi alivyojituma hususan katika kipengere kigumu alichocheza cha mgonjwa wa akili.

“Shaykaa alicheza kama mgonjwa wa akili nafasi ambayo ni ngumu sana lakini kwa uwezo wake aliitendea vyema nafasi hiyo na kufanikisha filamu hiyo kuwa na ubora wa kimataifa na kuiwezesha kushinda tuzo hiyo.

“Nampongeza sana Shaykaa kwa filamu hiyo ya Uhuru na gharama zake na namsisitiza kujituma zaidi ili apasue zaidi anga la kimataifa.

“Pamoja na Shaykaa nawasisitiza na wasanii wengine kujituma zaidi ili nchi yetu izidi kujitwalia tuzo kama hizo kila kukicha na kuipa sifa nchi yetu”. Alisema Nilesh.

Msanii Chiki Mchome akimpongeza Shaykaa na kuwataka wasanii wengine kuiga juhudi zake.

Wakati hafla ya kumpongeza Shaykaa ikiendelea msanii wa Bongo Muvi, Mike Sangu naye alipata nafasi ya kuzungumza ambapo alimpongeza msanii huyo na kusema tukio limeanza kurudisha heshima kwa filamu za kibongo.

“Tukio hili limeanza kurudisha heshima yetu wasanii wa filamu za kibongo ambayo awali tulionekana kama tumeshapotezana”. Alisema Mike.

Muigizaji Mike Sangu akimpongeza Shaykaa kwa jitihada zake za kurejesha heshima kwenye tasnia hiyo.

Msanii mwingine wa Bongo Muvi aliyetoa pongezi kwa Shaykaa ni Chiki Mchome ambaye aliwaomba wasanii wengine wa tasnia hiyo kumuunga mkono msanii huyo kwa kufuata nyayo zake.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dkt. Kiango Kilonzo akimkabidhi bendera ya taifa Shaykaa ambaye anatarajiwa kwenda kukabidhiwa tuzo yake Desemba 18 mwaka huu huko Dubai U.A.E

Baada ya kukabidhiwa bendera hiyo Shaykaa naye aliwapongeza Watanzania kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha mafanikio yake hayo kufikia kushinda tuzo hiyo.

Shaykaa na wadau wenzake wa filamu wakiwa na bendera hiyo baada ya kukabidhiwa.

Shaykaa pia aliishukuru Kampuni ya Pilipili Entertainment iliyomuandalia filamu hiyo iliyokidhi viwango vya kimataifa na kushinda tuzo hiyo yenye sifa kubwa ulimwenguni.

Leave a Comment