×

Spoti Xtra Laendelea Kumwaga Zawadi kwa Wasomaji

Adinan Rajabu akikabidhiwa zawadi yake na Mhariri Msaidizi wa Spoti Xtra, Martha Mboma.

GAZETI bora zaidi la michezo hapa nchini, Spoti Xtra, limezidi kuwapa tabasamu wasomaji wake kwa kuzidi kugawa zawadi mbalimbali kupitia chemsha bongo inayoendeshwa na gazeti hilo.

 

Hii ni wiki ya tatu washindi mbalimbali wanajishindia zawadi kemkem za chemsha bongo hiyo ambayo Spoti Xtra inashirikiana na wauzaji wa vyombo vya ndani, Vunja Bei Mobileshop.

 

Leo Jumamosi, Adinan Rajabu, mkazi wa Buza ambaye aliibuka mshindi wa wiki hii, alikabidhiwa zawadi yake katika Ofisi za Global Publishers zinazochapisha gazeti hili, zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

 

Adinan amefanikiwa kujishindia seti ya glasi baada ya kujibu kwa usahihi swali la wiki hii lililokuwa likiuliza hivi; KIJARIDA CHA NDANI YA BOKSI KINAPATIKANA KWENYE GAZETI LA LINI? Huku jibu lake likiwa ni GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI.

 

Akizungumza na Spoti Xtra baada ya kukabidhiwa zawadi yake hiyo, Adinan alisema: “Nina furahi kuwa mmoja kati ya washindi kupitia gazeti bora la michezo hapa nchini la Spoti Xtra, kama mdau mkubwa wa magazeti ya michezo ya Global Publishers ambayo ni Spoti Xtra na Championi, nashukuru kwa zawadi hii.

Wahariri na Waandishi wa Spoti Xtra wakiwa na mshindi wa Chemsha Bongo ya Spoti Xtra, Adinan Rajabu (katikati)

“Mimi ni shabiki wa Yanga, klabu ambayo ninaipenda sana kiasi cha kuitwa Shabiki wa Yanga lialia.

 

“Nawashauri wadau wengine wa mchezo wa soka kununua magazeti ya Spoti Xtra na kushiriki kwani kwa shilingi 500 tu niliyotoa nimeweza kujishindia zawadi hii kubwa. Hizi zawadi hazina longolongo wala kujuana, ukishinda tu unajipatia zawadi yako.

 

“Kama shabiki wa Yanga najivunia kupata taarifa za maendeleo ya timu yangu kupitia Spoti Xtra, kama mnavyojua tunaongoza ligi na kiukweli tuna jambo letu msimu huu.

 

Naye Mhariri Msaidizi wa Spoti Xtra, Martha Mboma ambaye alimkabidhi zawadi mshindi huyo, alisema: “Kama mnavyojua kuwa Gazeti la Spoti Xtra ndilo linaloongoza hapa nchini kwa ufanisi wa habari zinazoandikwa pamoja na uhakika wa takwimu.

 

“Wakati huu tumekuja na chemsha bongo hii ambayo inapatikana kwenye magazeti yote ya Spoti Xtra, hivi sasa Spoti Xtra linatoka JUMANNE, ALHAMISI na JUMAPILI.”

 

Spoti Xtra na Vunja Bei Mobileshop, wanashirikiana kwenye chemsha bongo hiyo ambayo inapatikana katika ukurasa wa pili wa Gazeti la Spoti Xtra.

 

Chemsha bongo hiyo inatoa zawadi kemkem ikiwemo friji, micro wave, Brenda, rice cooker, glasi, dinner set na vingine vingi.

 

Ili kujishindia zawadi hizo, unachotakiwa ni kununua Gazeti la Spoti Xtra ambalo kwa sasa linatoka mara tatu kwa wiki, JUMANNE, ALHAMISI na JUMAPILI kwa Sh 500 tu, kisha funua ukurasa wa pili utakutana na maelekezo ya kushiriki. Ukishinda, utapigiwa simu na kupewa maelekezo ya namna ya kujipatia zawadi yako.

STORI: JOEL THOMAS

PICHA: JAMES MBILINYI

Leave a Comment