
MWIMBAJI Mkongwe aliyeitumikia Bendi ya Sikinde kwa miaka mingi, Hassan Bichuka, ameeleza Watanzania kupitia Global TV Online kuwa maradhi aliyoyapata yamempelekea kushindwa kufanya kazi kwa miaka 3 na kufanya hali ya maisha kuwa ngumu katika familia yake kwani hakuna kipato kinachoingia.