
IBADA ya kuaga mwili wa baba wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, Mzee Urban Costantine Ndunguru, aliyefariki dunia juzi alfajiri, imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wa serikali, dini, siasa, ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji wengine wamejitokeza kuuaga mwili wa Nduguru kanisani hapo.
Baadhi ya viongozi waliofika ni Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Aboubakary Kunenge, Spika Mstaafu Mama Anne Makinda, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar, SACP Lazaro Mambosasa na wengine.
Akitoa neno la shukrani, Jokate amesema, “Baba yetu tulikuwa tunamwogopa sana, alikuwa ni mkali, ugonjwa ulikuja na baraka, alikuwa zaidi nyumbani tukaweza kufahamiana, lakini kumuogopa kule kulitujengea nidhamu ambayo imetufanikisha kufikia malengo yetu na leo kama watoto tunaweza kumuaga baba yetu kwa heshima.”