![]()
MADAKTARI wanaofanya kazi kwenye hospitali za umma nchini Kenya, wameungana na wahudumu wengine kwenye mgomo kulamamikia kutopewa bima ya afya na kufanya kazi kwenye mazingira magumu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa hilo linapitia changamoto ya janga la virusi vya Covid-19.
Mgomo huu unakuja baada ya mazungumzo kati ya wawakilishi wa madaktari na serikali nchini humo kugonga mwamba.
Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe, ametishia kuwafuta kazi wahudumu walioamua kugoma, mgomo huu unakuja wakati nchi hiyo inapoendelea kukabiliana na janga la Corona.
Kufikia sasa Kenya imerekodi visa 94,500 vya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya visa vipya 349 kuthibitishwa na vifo 1,618, baada ya watu wengine sita kuthibitishwa kufariki dunia kutoka na janga hilo hatari.