×

Jafo Ataka Wakurugenzi wa Halmashauri Nne Kujieleza

Waziri JafoWAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, leo Desemba 21, 2020, ameagiza wakurugenzi wa halmashauri nne za Msalala, Kahama, Korogwe na Sikonge, kutoa maelezo kwa nini hawakuwaruhusu walimu kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa).

 

Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa umoja huo leo jijini Dodoma na kueleza kuwa serikali ilitoa kibali cha mkutano huo kwa sababu wanaamini malengo makuu ya kiserikali yatawafikia walengwa wanaohudhuria lakini wakurugenzi hao walishindwa kutoa kibali kwa walimu husika kwenda kupata maelekezo ya serikali.

 

“Anatokea mkurugenzi anakataa kutoa kibali kwa hawa wapiganaji wa Dkt. John Magufuli… namuagiza katibu mkuu apate maelezo ya hawa,” alisema Jafo akitaka jambo hilo lifanyike mara moja.

Leave a Comment