
Miradi ya Premier imetoa msaada wa chakula, vinywaji, vifaa vya chooni, madaftari na vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kwa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Hidaya Orphanage Centre kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam.
Kituo cha kulelea watoto yatima Tanzania kimepokea msaada muhimu ambao utawawezesha kuendesha kituo hicho kwa miezi ijayo.
Miradi ya Premier ni kitengo cha hisani kwa jamii kwenye Kampuni ya michezo ya kubashiri, Premier Bet. Dhumuni lao ni kurudisha/kujitolea kwa jamii kupitia misaada kama hii.

Mzungumzaji wa huu Mradi huu Eric Kirita alisema: “Tunafuraha sana kuwa hapa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima, Hidaya Orphanage Centre, kuwapa zawadi hizi muhimu kwenye msimu wa Christmas. Kazi mnayoifanya kwa hawa watoto wasiojiweza ni ya kupendeza na tuna furaha sana kuweza kusaidia”.
“Huu ni muda wa mwaka wa kuwaza kuhusu wengine na tunaamini kila mtoto anastahili kusherehekea na kufurahia sikukuu ya Christmas.”
Kituo cha kulelea watoto yatima cha Hidaya kipo eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam. Kituo kimekua nyumba ya watoto 50, wenye umri kati ya miaka 6-17.
Pamoja na kuwapatia vitu vitakavyowasaidia hadi Mwaka mpya, Mradi wa Premier pia umeandaa chakula cha mchana kwa ajili ya watoto na wafanyakazi.
Mzungumzaji wa kituo cha kulelela watoto yatima cha Hidaya Ndugu Rashid S. Rashid alizungumza: “Tunatoa shukurani sana kwa Miradi ya Premier kwa msaada huu wa ukarimu na chakula cha mchana wa sikukuu ya Christmas. Jitihada zao zimeweka tabasamu katika nyuso za watoto wetu.”
Hii si mara ya kwanza kwa Miradi ya Premier kutoa kwa ajili ya Jamii ya Tanzania. Mwaka uliopita, walitoa msaada kama huu kwenye kituo cha kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam.
Mwezi ulioisha mradi huu wa Premier Project, ulilisaidia kwenye Utunzaji wa Mazingira kwa upandaji wa miti jijini Dodoma.
Kufahamu Zaidi kuhusu Miradi ya Premier, tafuta PremierProjectsAfrica kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook na Instagram.