
KAMA ulichukulia masihara kauli ya mabosi wa Yanga kuwa msimu huu wanalitaka kombe la ligi, basi utakuwa umejidanganya kutokana na kile ambacho mabosi wa timu hiyo wamekiamua.
Wakati huu wa dirisha dogo la usajili, mabosi hao kuonyesha kwamba hawataki mchezo, wameamua kuweka kando shilingi milioni 500 zitakazotumika kwa ajili ya kushusha vifaa ambavyo vitaongeza makali ndani ya kikosi hicho.
Kitita hicho kimetengwa na Yanga kwa ajili ya kupata saini za straika Steven Sey anayekipiga Namungo FC aliyejizolea umaarufu kutokana na staili yake ya kuchomekea kisha kupunga mkono kwa wapinzani wake, kila anapofunga bao, staili ambayo imekuwa ikiwakera sana wapinzani.
Pia mkwanja huo unaweza kutumika kama chambo ya kuwapata straika Mkongo Dark Kadima, Mnyarwanda Jacques Tuyisenge na beki Edward Charles Manyama.
Habari za ndani kutoka Yanga ambazo zimethibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, ni kuwa wametenga kitita hicho kwa ajili ya kuboresha kikosi hicho kwa kumsajili mchezaji yeyote kwenye kipindi hiki cha dirisha dogo.
“Tunataka kuboresha kikosi kwa kipindi hiki cha dirisha dogo na tayari kuna kiasi kikubwa cha fedha kwa makadirio
WILBERT MOLANDI NA SAID ALLY, Dar