×

Panga la Simba SC Lapita na Mastaa…

BAADA ya juzi Jumatatu, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez kuweka wazi kuwa wapo wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, baada ya wachezaji hao kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara, hatimaye majina manne ya nyota hao yamebainika.

 

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinadai kuwa wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo ni Miraji Athuman (Sheva) anayehusishwa na Namungo FC, Charles Ilafya na David Kameta ‘Duchu’ wanaotajwa kupelekwa Ihefu na Coastal Union na Kennedy Juma ambaye bado haijafahamika anakwenda timu gani.“

Uongozi unaona ni bora wakamalizie msimu kwenye timu ambazo watacheza mara kwa mara na kukuza viwango vyao kabla ya kurejeshwa tena kwenye timu.”

 

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa pia ni mshauri binafsi wa mwekezaji wa timu hiyo Mohamed Dewji ‘Mo’, Crescentius Magori ili kupata chochote juu ya ishu hiyo ambapo alisema: “Mimi siyo kiongozi wa Simba siwezi kuzungumzia hilo suala, watafute wenyewe wazungumze.”

 

Akizungumzia mipango ya usajili ya klabu ya Simba wakati huu wa dirisha dogo Barbara alisema: “Tupo kwenye usajili wakati huu wa dirisha dogo la usajili, kuna wachezaji ambao tunapanga kuwasajili, lakini pia wapo watakaotolewa kwa mkopo kipindi hiki.”

Leave a Comment