
UONGOZI wa Klabu ya Yanga kupitia kwa mjumbe wa Kamati ya Usajili, Eng Hersi Said, hatimaye imekamilisha dili la beki wa kati wa Polisi United, Idd Mobby ambaye sasa anapishana na aliyekuwa beki wa zamani wa Yanga, Kelvin Yondani aliyesajiliwa na klabu hiyo.
Yanga imekuwa kwenye mazungumzo na Mobby kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa, jambo ambalo liliwafanya kumwambia atulie na kwamba watamalizana naye mapema tu.
Chanzo chetu makini kimebainisha wazi kuwa, tayari Yanga wamekamilisha dili hilo na Polisi Tanzania, ambapo wamewawezesha fedha za kuipata saini ya Kelvin Yondani jambo linalowafanya wamuachie Iddi Mobby aungane na Yanga.“
Hadi muda huu tayari tuna uhakika sasa wa kuipata saini ya Idd Mobby kwani mwanzo tulifanya naye mazungumzo tu lakini hatukuweza kuwa na uhakika naye kutokana na Polisi kusuasua kumuachia, ila kwa kuwa tumefanikishia kumpata Yondani ni dhahili na wao wamekubali kumuachia aje kuungana nasi,” kilisema chanzo hicho.

Akizungumza na gazeti hili, Mobby alisema: “Ni kweli Yanga nimeshazungumza nao na tumemalizana, hivyo waliniambia nisubirie muda wowote watamalizana na klabu yangu ya Polisi.”
Hivi karibuni gazeti hili lilimkariri Eng. Hersi Said akisema: “Tunaleta mchezaji mmoja ambaye tupo kwenye hatua za mwisho za kumsajili, naweza kusema atakuwa mchezaji mwenye uwezo sahihi maana tunataka mchezaji ambaye ataingia moja kwa moja kwenye mipango ya kocha wetu baada ya kuwatoa baadhi kwa mkopo.”
Yondani mambo safi Polisi Naye, Ofi sa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema: “Mazungumzo kati yetu na Yondani yanaendelea na sasa tupo katika hatua za mwisho.“Tunahitaji kuimarisha kikosi chetu kwa kusajili wachezaji watakaoisaidia timu, mambo yakikamilika tutaweka wazi usajili wake na muda tuliomsainisha.
Stori na Musa Mateja na Khadija Mngwai,