×

Wabunge Republican Wafungua Kesi Dhidi ya Makamu Rais

WAKIWA na lengo la kupindua matokeo ya uchaguzi wa Marekani, mbunge wa baraza la wawakilishi, Louie Gohmert, na wenzake wa Republican, Jumatatu Desemba 28, 2020, walifungua kesi ya madai dhidi ya Makamu wa Rais, Mike Pence, ambaye ataongoza mkutano ujao wa Bunge  utakaokamilisha ushindi wa Rais Mteule kutoka chama cha Democratic, Joe Biden.

 

Madai hayo, ambayo mwenyekiti wa chama cha Republican wa jimbo la Arizona, Kelli Ward na wenzake pia wamejiunga nayo, yataangalia uwezo wa Pence kama makamu wa rais, ambapo sheria ya kuhesabu kura ya 1887 inasema anapaswa kuongoza mkutano mkubwa wa Januari 6 wa Bunge kuhesabu kura za uchaguzi na kuhitimisha ushindi wa Biden dhidi ya rais wa sasa, Donald Trump.

 

Madai yanamtaka jaji wa mahakama ya Texas, Jeremy Kernodle, kumpa Pence mamlaka ya kipekee na uhuru pekee wa kuamua ni kura zipi za uchaguzi kutoka jimbo fulani zinapaswa kuhesabiwa.

 

Madai hayo yanasema sheria ya kuhesabu kura imekiuka marekebisho ya 12 ya Katiba ya Marekani, ambayo yanasema Mwenyekiti wa Seneti mbele ya wabunge wa seneti na Baraza la Wawakilishi, atafungua vyeti vyote halafu kura ndipo zitahesabiwa. Nchini Marekani makamu wa rais anatumuka kama Mwenyekiti wa Seneti.

Leave a Comment