×

Piere Liquid Apata Kigugumizi; Pombe na Mke Nani Zaidi?

MCHEKESHAJI, Piere Likwidi, amesema hawezi kuacha kunywa bia kwa sababu watu wengi wamemjua kwa ‘style’ hiyo ya unywaji ila endapo itatokea mke wake atamkataza basi atajaribu kumsikiliza ili kuona kama itawezekana.

 

Akihojiwa na moja ya vyombo vya habari, amesema hawezi kuacha pombe kwani hajizamletea madhara yoyote ila kama mke wake akimkataza atapunguza kunywa ila siyo kuacha kabisa.

 

“Kusema ukweli mimi siwezi kuacha kwa sababu hivi vitu mimi havijaniletea madhara yoyote ya kunidhuru au kuniathiri, na watu wengi wamenifahamu kupitia hivyo.  Kama mke wangu hapendi, nitapunguza kunywa na nitamsiliza kwani ndani ya nyumba kunahitajika maelewano na makubaliano ili kufikia muafaka,” amesema.

 

Aidha ameongeza kusema bado hajajaliwa kupata mke ila ana mwanamke ambaye anaishi naye na wana muda wa mwaka mmoja mpaka sasa.

Leave a Comment