×

Wahariri Na Waandishi Wavutiwa Na Makumbusho Ya Olduvai Gorge, Ngorongoro

Mhariri Mwandamizi wa Magazeti ya Global Publishers, Elvan Stambuli (kulia) akipokea cheti kutoka kwa Dk Christopher Timbuka, Naibu Kamishna Uhifadhi, Maendeleo ya Jamii na Utalii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) baada ya ya kushiriki semina ya siku tatu ya wahariri wa vyombo vya habari na waandishi waandamizi kuhusu uhifadhi wa Ngorongoro Crater iliyoandaliwa na kufanyika katika makao makuu ya hifadhi hiyo, Karatu Mkoani Arusha kwa lengo la kubadilishana mawazo na kushauriana juu ya changamoto za uhifadhi wake.
Mwandishi Mwandamizi wa ITV na Radio One, Farhia Middle akipokea cheti cha ushiriki wa semina hiyo kutoka kwa Dk. Christopher Timbuka.
Mwandishi wa Habari wa ITV Arusha, Beatrice Gerald akipokea cheti cha ushiriki wa semina kutoka kwa Dk. Timbuka.
 Afisa Urithi wa Utamaduni wa Makumbusho ya Olduvai Gorge, Godfrey Ollemoith akitoa maelezo kwa wahariri na waandishi wa habari wakati walipotembelea katika eneo hilo ikiwa ni moja ya mafunzo ya uhifadhi wa mazingira katika hifadhi ya Ngorongoro.
Mwandishi wa habari wa BBC, Abubakar Famau akiongozana na blogger mwandamizi Ahmed Michuzi kutoka Michuzi Media Group mara baada ya kutembelea makumbusho hayo na kuona mambo mbalimbali.
Ollemoith akitoa mada na kujibu maswali kwa wahariri na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea makumbusho hayo.
Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Joyce Mgaya akizungumza jambo wakati wa semina hiyo.
Dk Timbuka akizungumza na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari katika makumbusho ya Olduvai Gorge mara baada ya wahariri hao kutembelea katika makumbusho hayo.

Wahariri wa vyombo vya habari na waandishi waandamizi wametembelea hifadhi wa Ngorongoro Crater baada ya ya kushiriki semina ya siku tatu ya wahariri wa vyombo vya habari na waandishi waandamizi kuhusu uhifadhi wa Ngorongoro Crater iliyoandaliwa na kufanyika katika makao makuu ya hifadhi hiyo Karatu Mkoani Arusha kwa lengo la kubadilishana mawazo.

Leave a Comment