×

Serikali Yatangaza Awamu ya Pili Ya Ajira 5000 za Walimu

Serikali imetangaza Awamu ya Pili ya ajira kwa Walimu 5,000 ili kufikia idadi ya Walimu 13,000 kutokana na kibali kilichotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.

 

Akihutubia Mkutano wa Pili wa Umoja wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi #Tanzania Bara, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Joseph Nyamhanga amesema, Awamu ya Pili ya ajira hizo itafanyika mapema mwaka huu.

 

Awamu hiyo ya Pili inafanyika baada ya ajira za Awamu ya Kwanza 8,000 kuripoti kazini. Walimu hao 5,000 watapelekwa Vijijini na kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa.

Leave a Comment