Breaking: Kocha wa Simba Abwaga Manyanga
UONGOZI wa Klabu ya Simba umetangaza rasmi kuachana na kocha wake mkuu, Sven Vandenbroeck, kwa makubaliano ya pande mbili.
Nafasi ya Sven itakaimiwa kwa muda na kocha msaidizi wa Simba, SelemanI Matola, mpaka atakapotangazwa kocha mwingine.