×

Simbachawene Ampa Sirro Siku 7 Kushughulikia Bajeti ya Mbwa – Video

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (wa pili kulia), akimwangalia Askari Mbwa wa Kituo cha Polisi Bandari, jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara katika kikosi hicho, jana.  Wa tatu kulia ni Msimamizi wa Askari Mbwa hao, Richard Mshuza, akitoa maelezo ya kazi anazofanya Mbwa huyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amempa siku saba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Simon Sirro, kushughulikia bajeti ya chakula cha mbwa wawili wanaotumika kulinda ulinzi na usalama.

 

Simbachawene ametoa agizo hilo jana Ijumaa Januari 8, jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kikazi alipotembelea maeneo ya Jiji hilo.

 

Amesema mbwa hao wawili kati ya saba hawana bajeti ya chakula hivyo wanatakiwa kupewa bajeti kwa sababu wanafanya kazi kubwa kuliko binadamu.

 

“Mbwa hawa ni askari wanaotumika sana ni nimemwagiza IGP ndani ya siku saba ahakikishe mbwa wote saba wapo kwenye bajeti.

 

“Katika mbwa saba wapo mbwa watano wenye bajeti na wawili hawapo kwenye bajeti ambapo kwa mwezi wanatumia Sh. laki nane, na inatakiwa wote wawepo kwenye bajeti,” anasema Simbachawene

 

Aidha, Simbachawene amempa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa zawadi ya gari kama ishara ya pongezi kwa utendaji wake ikiwa na kudhibiti uhalifu na kupungua kwa kiasi kikubwa.

 

WAZIRI AWATETEA MBWA, ATOA MAAGIZO KWA IGP SIRRO – “NAKUPA SIKU 7, UTENGE BAJETI”

Leave a Comment