
NDEGE iliyokuwa na abiria zaidi ya 62 imepotea na haijulikani ilipo muda mfupi baada ya kuruka kutoka jJakarta, mji mkuu wa Indonesia.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737 ya Shirika la Sriwijaya ilipoteza mawasiliano ikiwa safarini kuelekea Pontianak katika mkoa wa Kalimantan Magharibi, maafisa wa anga wa nchi hiyo wamesema.

Tovuti ya ufuatiliaji wa ndege, Flightradar24.com, imebainisha kuwa ndege hiyo imepotea zaidi ya mita 3,000 kwa urefu chini ya dakika ambazo ni sawa na futi 10,000.
