×

Gari la Mabomu Karibu na Bunge Lakamatwa

POLISI jijini Washington DC, Marekani, wamekamata gari lililokuwa na mabomu na bunduki, likiwa limeegeshwa karibu na Bunge siku ya Jumatano wakati wafuasi wa Rais Donald Trump walipovamia jengo hilo.

 

Polisi wamesema mtu mmoja aliingia ndani  Bungeni akiwa na bunduki na risasi zaidi ya mia moja huku akiwaambia wenzake kuwa anataka kumpiga risasi Spika, Nancy Pelosi.

 

Aidha, kikosi cha kutegua mabomu kimesema mabomu kadhaa yamegunduliwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Washington. Wakatgi huohuo, watu  67 wamekamatwa na  13 wakifunguliwa mashtaka kufuatia tukio la kuvamia Bunge.

Leave a Comment