×

Waziri Afrika Kusini Apatikana na Corona

WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Rais nchini Afrika Kusini, Jackson Mthembu, amekuwa waziri wa nne katika serikali ya Afrika Kusini kupatikana na virusi vya corona.

 

Mthembu alipimwa virusi hivyo baada ya kuwa na dalili, ilisema ofisi ya rais. Amewekwa katika karantini na kila mtu aliyekaribiana naye. Waziri huyo ali-tweet mwenyewe akisema ana maumivu ya tumbo.

 

Afrika Kusini ina aina mpya ya virusi vya corona inayosambaa kwa kasi kubwa.

 

Nchi hiyo ilirekodi wagonjwa wapya 15,046 na vifo vipya 416, na kulifanya taifa hilo kufikia jumla ya wagonjwa wa corona 1,246,643 na vifo 33,579.

Leave a Comment