×

Matokeo ya Uchaguzi Uganda 2021: Museveni, Bobi Wine Wachuana Vikali

TUME ya Uchaguzi nchini Uganda siku ya Alhamisi Januari 14, 2021 ilihakikisha kwamba matokeo ya moja kwa moja ya Uchaguzi katika kituo kikuu cha kujumlisha kura cha kitaifa yatendelea licha ya kufungwa kwa intaneti nchini humo.

 

Mkuu wa Tume ya Uchguzi, Simon Byabakama alisema kwamba wanatumia mbinu fulani kurusha matokeo hayo lakini haikutoa maelezo zaidi.

 

‘’ Hatutumii intaneti ya nchini kurusha matangazo . Tunatumia mfumo wetu . Musijali, matokeo yatapeperushwa licha ya kwamba mtandao umefungwa’’ , aliambia waandishi.

 

Ilitoa matokeo ya awali siku ya Ijumaa kutoka vituo 330 ambayo yalimuonesha rais Yoweri Museveni akichukua uongozi wa mapemakulingana na gazeti la daily Monitor.

 

Taifa hilo lina jumla ya vituo vya kupigia kura 34,684

Sheria ya Uganda inaipatiauwezo Tume hiyo kupokea matokeo kutoka wilaya zotena kuyatangaza katika muda was saa 48 baada ya shughuli ya kupiga kura kukamilika.

Leave a Comment