×

Jeshii la Polisi Kumchunguza Cristiano Ronaldo

 

MSHAMBULIAJI wa Juventus, Cristiano Ronaldo, anachunguzwa na maafisa wa polisi wa Italia kuhusu safari aliyokwenda ili kusherehekea siku ya kuzaliwa na mpenzi wake ambapo  anatuhumiwa  kuvunja masharti ya Covid -19 kwa kusafiri kati ya Jimbo la Piedmont na Valle d’Aosta.

 

Picha zilizochapishwa na baadaye kuondolewa mtandaoni zinawaonyesha wawili hao wakiwa katika hoteli moja siku ambayo Georgina Rodriguez alisherehekea kuwa na umri wa miaka 27.

 

 

Italia imeshuhudia mamia ya vifo na maelfu ya maambukizi mapya kila siku ambapo taifa hilo liliathiriwa vibaya mapema wakati wa mlipuko huo mwaka uliopoita na sasa liko katika wasiwasi wa ksiasa baada ya kushindwa kupunguza idadi maambukizi katika wimbi la pili la maradhi hayo.

 

 

Ripoti nchini Italia zinadai kwamba wawili hao walisafiri siku ya Jumanne na kusalia katika mgahawa huo usiku kucha kabla ya kurudi Turin, nyumbani kwa klabu ya Serie A Juventus siku ya Jumatano.

 

 

Utata huo unajiri miezi kadhaa baada ya Ronald kuambukizwa corona ambapo wakati huo alikosolewa na waziri wa michezo nchini Italia kwa kwenda Portugal ili kushiriki katika mechi ya kimataifa muda mfupi kabla ya kupatikana na maambukizi ya ugonjwa huo.

 

 

Leave a Comment