×

Avuliwa Ukuu wa Shule kwa Tuhuma Kuiba Vifaa vya Ujenzi

MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimb,i amemwagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Singida, Rashid Mwandoa, kumvua cheo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwachambia, Edward Ighonde, na Mwalimu Mkuu Msaidizi, Charles Mtiko, kwa tuhuma ya wizi wa vifaa vya ujenzi wa nyumba ya walimu.

 

Vifaa vinavyodaiwa kuibiwa ni mbao za kupauliwa, saruji na nondo ambayo thamani yake bado haijafahamika. Nchimbi ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo ya ujenzi ambapo watuhumiwa wote wako polisi.

 

Aidha ametoa maagizo kwa viongozi kuacha tabia ya kuwatetea watumishi wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu na atakayebainika atashughulikiwa vilivyo.

Nchimbi amewataka viongozi wa serikali kusimamia miradi na kuwa waaminifu katika fedha zinazoletwa na serikali ya Rais Magufuli pia wananchi wahakikishe wanalinda mali hizo kwani miradi hiyo ni kwa ajili ya maendeleo yao.

Leave a Comment