
Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga, Twaga Sultan na Abeid Ismail wakazi wa jijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa Mawili yote yakiwa ni yakiktwa wakisafirisha dawa za kulevya kg 26.86 aina ya bangi.
Watuhumiwa hao wamesomewa mashtaka Yao na wakili wa serikali, Faraji Nguka Mbele ya Hakimu Mkazi Kasian Matembele ambapo wanadaiwa kukutwa na eneo la Sea Link Azam Bandarini mnamo Januari 6, 2021 wakisafirisha bangi.
Baada ya kuwasomea mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao wamekana kutenda makosa hayo na hakimu akasema kutokana na sheria za dawa za kulevya zinazozidi kilo 20 mtuhumiwa hawezi kupatiwa dhamana.
Hivyo hakimu ameahirisha kesi hiyo hadi februali 15 mwaka huu.
Upande wa utetezi ukiingozwa na wakiki Hekima Mwasipu umeomba mahakama kwa kuwa watuhumuwa wamekutwa na udhibiti upelelezi uharakishwe.
“Mheshimiwa hakimu naomba upande wa mashtaka kwa kuwa umewakuta washtakiwa na vidhibiti hivyo ninaomba upelelezi usichukue mda ili kesi iweze kuendelea,” alisema.