×

Breaking News: Lori la Mizigo Laungua Moto Kimara – Dar (Video)

TAARIFA zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa lori la mizigo limeungua kaa moto, majira ya saa 4:45 usiku huu wa Januari 26, 2021, maeneo ya Kimara – Korogwe, wakati lori hilo likiwa katikati kabisa mwa Barabara Kuu ya Morogoro na kuzua taharuki miongoni mwa wananchi waliokuwa katika eneo hilo.

 

Kwa mujibu wa ripota wetu aliyekuwa eneo la tukio wakati moto huo unaanza kuwaka, ameeleza kuwa, baada ya kuonekana viashiria vya moto huo kwenye kibeni ya gari, dereva na wenzake walishuka haraka na kuanza kumwaga mchanga huku wakipiga simu kuomba msaada wa kikosi cha zimamoto, lakini mchanga huo haukusaidia chochote, wananchi waliokuwa eneo hilo walipata wazo la kuomba maji kwenye nyumba zilizopo pembezoni mwa barabara hiyo ambayo yalisaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya moto huo kuwaka.

 

Hata hivyo, walifanimiwa kuomba mitungi ya zimamoto (fire extinguisher) kutoka kwa madereva wa magari yaliyokuwa kwenye foleni eneo hilo la tukio ambazo zilisaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza moto huo.

 

Hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa kutokana na ajali hiyo lakini gari ndilo limeharibika vibaya sehemu ya injini huku tela na mizigo yake (mchele uliokuwa umepakiwa) vikiwa salama.

 

Mpaka tunaondoka eneo la tukio, kikosi cha zimamoto kilikuwa hakijafika eneo la tukio huku kukiwa na foleni kubwa za magari yanayotoka mjini kuelekea maeneo ya Mbezi na Morogoro na yale yanayotoka Morogoro na Mbezi kuingia Mjini. Hii ni kutokana na barabara hiyo kushindwa kupitika kirahisi sababu ya ajali hiyo.‎

 

Leave a Comment