
ALIYEWAHI kuwa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, anaripotiwa kuishitaki timu hiyo mahakamani.Inadaiwa kuwa, Rweyemanu ambaye aliondolewa Simba mwaka jana baada ya Simba kupata matokeo mabaya mfululizo sasa inaripotiwa anataka kusafishwa na kulipwa fedha ambazo anaidai timu hiyo ili wamalizane vizuri.
Akizungumza na Championi Jumamosi, mwanasheria wake, John Feka, alikiri kuwepo kwa madai hayo ambayo yapo kwenye mahakama ya usuluhishi.
Feka alisema mteja wake ameitaka Simba kukanusha tuhuma zilizotolewa na timu ambazo zililenga kumchafua kwa makusudi.

Alisema kuwa, jana mahakamani viongozi hao wa Simba waliomba kufikia muafaka wa sakata hilo kwa kukaa pamoja kufikia muafaka mzuri ili kulimaliza hilo.
“Kweli kesi ipo mahakama ya usuluhishi na kikubwa ipo kesi ya madai ya fedha ambazo ni siri.“Kesi nyingine ya tuhuma ambazo amepewa mteja wangu zilitaka kumchamfua kutokana na tuhuma alizopewa,” alisema wakili huyo.
Stori: Careen OscarDar es Salaam