×

Mama Kiba Aanika Ukweli Ndoa ya Kiba na Amina ‘Kuvunjika’

 

MASHABIKI wengi wa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba wamekuwa wakitamani  kusikia kauli ya msanii huyo kuhusu tetesi za ndoa yake na mwanadada kutoka nchini Kenya, Amina, ambapo hatimaye mama mzazi wa Kiba ameamua kufunguka ukweli.

 

 

Mama huyo ambaye hajazoeleka kwenye media amesema kuwa mkwe wake, Amina yupo likizo ya mapenzi, Mombasa nchini kwao Kenya.

 

Ameongeza: “Amina ni mtu mzuri sina ugomvi na yeye, nashangaa watu wanaongea mitandaoni nyumba ina watu wengi hadi Amina anashindwa kukaa, nina watoto wanne hao wengine wanatoka wapi? Naishi Kariakoo lakini kwa sasa naishi Tabata kwa Alikiba.

 

 

“Sipendi Instagram kwa sababu sioni faida yake, siwezi kutumia umaarufu wa wanangu kupata umaarufu, watoto wangu sio wabishi wananisikiliza.”

 

 

Leave a Comment