×

Apple Music yaja na Isgubhu, Dansi ya Kiafrika

APPLE Music imezindua Isgubhu, ikiwa ni hatua ya kukamilisha taswira halisi ya kile kiitwacho Africa’s Dance and Electronic Music, kwa maana ya dansi ya Kiafrika na Muziki wa Kielekroniki.

 

Muziki huo unaotingisha dunia hivi sasa, umetawala aina ya uchezaji kiasi cha miongo kadhaa iliyopita, na Apple Music hivi sasa imedhamiria kuzionyesha kwa kuziinua kazi za ma-DJ, maprodyuza na wasanii katika anga za sasa.

 

“Apple Music kwa muda mrefu imewaunga mkono ma-DJ mahiri, wasanii na maprodyuza katika jumuia ya muziki wa dansi na muziki wa kielektroniki barani Afrika na tuna furaha kubwa katika kuzindua Isgubhu.

 

“Timu zetu za kikanda ndiyo watetezi wetu wa kweli wa utamaduni husika na tumedhamiria kuendelea kuwaunganisha wasanii katika macho ya walimwengu,” anasema Stephen Campbell, Mkuu wa Kitengo cha muziki wa Dansi na Muziki wa Kielektroniki wa Apple Music.

 

Isgubhu, neno la kabila la Kizulu linalomaanisha ‘mdundo’ au ‘mapigo’ linalotumiwa katika kuonyesha muziki wenye kuunguruma au wenye mlio mkali wa juu, linatoa heshima kubwa katika mitindo mbalimbali ya muziki na wasanii wa Afrika ambao wameshiriki kikamilifu katika kujenga taswira ya muziki huo, duniani kote.

 

Kazi imeanza kuanzia kwa magwiji wa Afrika Kusini kama Black Coffee, Prince Kaybee, Black Motion na DJ Lag, maprodyuza wa Kenya, Euggy na Slikback hadi kundi maarufu la Uganda la Nihiloxica.

 

“Ni heshima kubwa kwangu, kutajwa kama msanii wa kwanza wa shujaa wa Isgubhu na marafiki zangu kwenye Apple Music. Kwangu, nyumbani ni kila kitu… msingi wa maisha yangu. Kupeleka sauti za Afrika Kusini ulimwenguni ni jambo lenye thamani na maana sana kwangu, kamwe sitaacha kuifuatilia,” anasema Black Coffee.

 

Mitindo kadhaa ya muziki itaimarika chini ya uongozi wa Isgubhu ikiwemo ile ya Gqom, Amapiano, Kwaito, Mzansi House, Deep House na Shangaan Electro, pamoja na sehemu ya albamu maarufu ambazo zitatoa sura halisi ya albamu za Dansi ya Kiafrika na Muziki wa Kielektroniki ili kuzipa ubunifu rahisi.

 

Akizungumzia kuhusu hilo, DJ Lag alisema: “Albamu hizi ndizo zilizonijenga na kunipa umaarufu. Wimbo kama ‘Undisputed’ wa Big Nuz, ulinipa matumaini makubwa kuhusu matumaini yangu kuwa prodyuza siku moja, wakati huo nikiwa na umri wa miaka 14 tu.

 

“Ninaupenda muziki wa dansi wa Afrika Kusini na nafikiri tuna mazingira ambayo yanazidi kuimarika na kuleta ubunifu zaidi kila baada ya miaka michache.

 

“Kwaito, Afro House, Gqom, Amapiano ni harakati zinazojumuisha watu wengi na si mtindo wala muziki tu.”
Isgubhu pia itajumuisha chaguo maalum la ma-DJ kutoka sehemu maarufu zaidi za bara hili, wakiwemo: DJ Zinhle, Caiiro, Kabza De Small, Kyle Watson, Stiff Pap, DBN Gogo, Da Capo, Gina Jeanz na wengine.

Tazama Isgubhu kupitia Apple Music http://apple.co/Isgubhu

Na Mwandishi Wetu

Leave a Comment