
HABARI ya mjini kwa sasa ni Tamthiliya ya Pazia, inazidi kuwashika mashabiki wa tamthiliya kutokana na kisa chake cha kusisimua.
Katika episode ya 13 hadi 15 kwenye PAZIA tuliona mambo mengi yalitokea. Kwanza; Eliza ambaye ni mama yake na Groly anamwambia Heri ukweli kuwa matatizo ya Regina yote ni mpango wa mwanaye Groly na sio Edu kama wanavyodhani.
Hivyo, anamuomba apinge ndoa ya Edu na Regina na yeye atamsaidia kumsomesha Regina Chuo Kikuu huku Jemo na Regina wanaonana na Jemo anamwambia Edu amempiga picha za uchi hvyo atazitumia kama kigezo cha kusitisha hiyo ndoa lakini Regina anasema hajali chochote.

Edu naye tunamuona ana mawazo sana lakini anapata bahati ya kushinda milioni 100 za bahati Nasibu.
Jemo naye tunamuona akipanga mipango ya kumuangamiza Edu ili ndoa yake ifeli.
Regina naye tulimuona amekata tamaa na kumwambia Edu kuwa ameamua amuachie uamuzi yeye achague amuoe ama lah ila cha ajabu safari hii Edu anamuonea huruma Regina na kukubali kwa hiari yake mwenyewe kuwa atamuoa Regina.
Jambo hilo la kukubali haraka harakata wakati tangu awali alikuwa hakubali, lilimfanya Regina asiamini na kuonekana kufurahi sana lakini baba yake na Regina anakataa katakata ndoa ya Regina na Edu.
Fred naye tunaona amepata taarifa ya wazazi wake wamepata ajali hivyo anatakiwa asafiri kwenda kuwaona na nauli hana, anamuomba Jemo lakini Jemo anakataa kumsaidia.
Cha kushangaza, Edu anaingiwa na huruma na kumsaidia hizo pesa wakati Edu anaondoka baada ya kumpa pesa Frad, majambazi wanamvamia na kumpiga risasi mbele ya Fred.

Siku ya harusi inafika, Regina anapiga simu ya Edu lakini haipokelewi huku Fred tukimuona anasafiri kwenda kwa wazazi wake nje ya nchi.
Muda wa kufunga ndoa umefika kanisani, bwana harusi haonekani. Glory anamuhisi kitu Jemo lakini Jemo anajifanya kama hajui kitu huku hospitali tunaona jopo la madaktari likipambania uhai wa Edu.
Regina anawasili kanisani lakini Edu bado hajafika ndipo Jemo anapojitokeza na kuomba yeye ndio afunge ndoa na Regina jambo linalowashangaza wengi. Regina alilipuka kwa hasira na kusema hawezi kufanya icho kitu.
Wakati huo huo Glory naye anataka kufunga ndoa na Jemo, hii harusi ilipata fedhea sana ndipo Regina alipoamua kuondoka kanisani baada ya kuona mambo hayaeleweki na tuliishia harusi imeshindwa kufungwa kwa kuwa bwana harusi hakutokea.

Wiki hii katika pazia tunaweza kuona Edu bado yupo hai na baada ya Regina kugundua hilo, anaenda hospitali kuomba ndoa yake ifungwe hospitali.
Kupata mwendelezo wa uhondo huu, nunua kifurushi chako cha Dstv utajionea uhondo nyumbani kwako kupitia channel ya Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Jumatano saa moja na nusu usiku, usikose!