
KIUNGO wa Azam FC, Frank Domayo, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mguu.
Domayo nje mwezi mmoja Domayo aliumia mguu kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe uliochezwa hivi karibuni na kumalizika kwa sare ya 1-1.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria, amesema: “Domayo atakaa nje kwa muda wa mwezi mmoja kwa majeraha ya mguu aliyoyapata kwenye mchezo wetu na TP Mazembe.”
Huyu ni kati ya wachezaji mahiri kwenye kikosi cha Azam kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akiitumikia timu hiyo uwanjani.
CAREEN OSCAR, Dar es Salaam