
MFALME wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba maarufu kama King Kiba, ambaye anafanya vizuri kwa sasa na ngoma yake “Infidèle” ambayo ndani ameimba baadhi ya mashairi kwa lugha ya Kifaransa, ameweka kambi nchini Nigeria mapema wiki hii ambapo atakaa kwa muda wa wiki mbili.
“Lagos for 2 weeks, Album almost done,” ameandika Alikiba kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Albamu hiyo mpya ya #AliKiba inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake, mpaka sasa haijafahamika itaitwaje, lakini tayari ameshaweka wazi nyota huyo kuwa itatoka kabla ya mwezi sita.