×

Marekani Yaiwekea Vikwazo Myanmar

 

RAIS wa Marekani, Joe Biden, ametangaza kuidhinisha amri ya kiutendaji ya kuwawekea vikwazo vipya wahusika wa mapinduzi ya kijeshi ya Myanmar na kusisistiza kurejeshwa demokrasia na kuwaachia viongozi wa kiraia.

 

Biden ametangaza kuidhinisha amri ya kiutendaji ya kuwawekea vikwazo vipya waliohusika na mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar na kurejelea wito wake wa kurejeshwa demokrasia na kuwaachia viongozi wa kiraia.

 

Amesema amri hiyo itawezesha utawala wake “kuwawekea vikwazo haraka viongozi wa kijeshi ambao walihusika na mapinduzi, maslahi yao ya kibiashara sambamba na jamaa zao wa karibu.”

Rais Biden ameongeza kuwa wiki hii Marekani itabainisha awamu ya kwanza ya wale wataoguswa na vikwazo hivyo na vilevile inawazuia majenerali nchini Myanmar kuweza kuzifikia mali zenye thamani ya dola bilioni 1 katika fedha za serikali ya Myanmar zilizoko Marekani.

 

Mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika  Februari Mosi ambayo yalimuondoa madarakani kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia, Aung San Suu Kyi, yalitokea chini ya wiki mbili zilizopita baada ya Biden kuapishwa na kuonekana kuwa mtihani wa mapema kwa kiongozi katika kushughulikia migogoro ya kimataifa.

Leave a Comment