×

Guardiola Awataka Messi, Ronaldo, Mbappe Man City

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema anatamani kuwa na mchezaji kama Lionel Messi, Cristiano Ronaldo au Kylian Mbappe kwenye kikosi chake, ili awe analeta utofauti, lakini anafuraha na kikosi chake cha sasa ambacho hakitegemei uwezo wa mchezaji mmoja.

 

 

Kocha huyo mhispania alisema hayo baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tottenham, ambao ulikuwa ni ushindi wa 11 mfululizo kwenye michezo ya ligi kuu England, na sasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 7.

 

 

Pep aliwasifu wachezaji wake kwa kuwa na muendelezo bora na kupata matokeo mazuri kwa kutotegemea uwezo wa mchezaji mmoja bali ubora wa timu kwa ujumla.

 

 

“Hatuna mchezaji anayeweza kutupa matokeo kwa uwezo wake binafsi, hatuna Messi, Cristiano, Mbappe au Neymar tunapaswa kupambana kama timu. Kiukweli ningependa kuwa na mchezaji ambaye anafunga kwenye kila mchezo mabao 4”, alisema Pep.

 

Manchester City walihusishwa kumuwania mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel Messi katika dirisha dogo la usajili, pindi mchezaji huyo alipoomba kuondoka katika klabu hiyo, lakini pia inatajwa Man City watapeleka ofa pindi mchezaji huyo bora wa dunia mara 6 atakapo maliza mkataba mwishoni mwa msimu huu na atakuwa mchezaji huru.

Leave a Comment