
MKURUNGENZI wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini (TMA), Dk Hamza Karelia, amesema mvua za masika kwa mwaka 2021 zinatarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya mwezi Februari.
Akizungumza leo Februari 18, Jijini Dar es Salaam, amebainisha kuwa mvua hizo zitaanza kunyesha hususani katika maeneo ya mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kaskazini mwa Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia.
Aidha,amesema mvua hizo zinatarajiwa kuisha mnamo wiki ya tatu ya mwezi Mei, 2021.