×

Kaze: Tuna Wakati Mgumu, Hatujiamini

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze raia wa Burundi, amefunguka kuwa kwa sasa kikosi chake kinapitia wakati mgumu kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bara.

 

Kaze ameongeza kwamba hali hiyo ya kuwa na wakati mgumu inatokana na nyota wake wengi kushindwa kujiamini kiasi wanakosa nafasi za wazi za kufunga mabao.

 

Katika mechi nne za mwisho za Ligi Kuu Bara, Yanga wameshindwa kupata ushindi baada ya kutoka sare dhidi ya Gwambina 0-0, Prisons 1-1, Mbeya City 1-1 na Kagera Sugar 3-3.

Kocha huyo ameliambia Championi Ijumaa, kuwa kikosi hicho kwa wakati huu kinapitia wakati mgumu kwa sababu ya kushindwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi zao.

 

“Ni kweli kuhusu hilo tumekuwa tukikosa nafasi za mabao mengi tu hata kwenye mechi na Kagera Sugar tulikuwa na nafasi zaidi ya mabao mawili.“

 

Suala hilo linafanya tukose hali ya kujiamini lakini kwa mtu yeyote au timu ile inaweza kupitia kwenye wakati huo, kwa sasa sisi tuko kwenye wakati huo mgumu. Ligi bado mbichi na ndefu tutaangalia kila ambacho hakipo sawa na tutafanyia kazi,” alimaliza Kaze.

Stori: Said Ally Dar es Salaam

Leave a Comment