×

Makamu Mkuu wa Sekomu Kuzikwa Kesho

Prof. Vincent Kihiyo, Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) aliyefariki dunia Februari 18 atazikwa kesho, Februari 20, 2021.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki limetangaza kuwa Marehemu atazikwa Kijiji cha Mhelo, Irente saa saba mchana. Alifariki katika Zahanati ya Mount Usambara, Lushoto Tanga alikokuwa akipatiwa matibabu.

Leave a Comment