Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi baada ya kuagwa leo Ijumaa, Februari 19, 2021, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam umesafirishwa na tayari umeshafika nyumbani kwao Korogwe, mkoani Tanga kwa ajili ya maziko yanayotarajiwa kufanyika kesho.