×

Silinde Amsimamisha Mkuu wa Shule Mtwara

NAIBU waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde amemsimamisha kazi mkuu wa shule ya sekondari ya Naliendele Halidi Mchanga kwa kushindwa kukamilisha mradi wa bweni na bwalo la chakula katika shule hiyo hiyo kwa wakati huku fedha walizopewa na serikali zimeisha na ujenzi ukiwa bado haujakamilika.

 

Naibu waziri Silinde amechukua uamuzi huo baada ya kutembelea shule hiyo iliyopo katika halmashauri ya manispaa ya Mtwara Mikindani mkoa wa Mtwara na kukuta matumizi mabaya ya fedha ambazo zilipaswa ujenzi huo uwe umekamilika toka mwishoni mwaka mwaka jana 2020 lakini umesimama baada ya fedha zote milion 180 zikiwa zimeisha huku majengo hayo yakiwa yamesimama.

 

Leave a Comment