×

Stendi Mbezi Luis Kuanza Kutumika Feb 25

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge, jana Februari 21,  amesema  kuwa stendi kuu ya mabasi ya mikoani ya Mbezi Luis itaanza kutumika rasmi Februari 25, 2021 kwa magari kuanzia safari katika kituo hicho, na kwamba kituo cha mabasi cha Ubungo kilichokuwa kikitumika awali hakitatumika tena.

 

Amesema hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa miundombinu yote muhimu ikiwemo majengo, maegesho, barabara na ofisi za kutoa huduma.

 

Aidha, amesema tayari serikali imekutana na wadau wote husika kikiwemo Chama cha Wamiliki wa Mabasi TABOA na wote wamejiridhisha kuwa kituo kimekamilika na kipo katika hali nzuri ya kutoa huduma, hivyo wapo tayari kutoa huduma.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Liana, amesema ifikapo siku ya Jumanne watafanya kikao na wafanyabiashara wote watakaokuwa wakitoa huduma ndani ya jengo na siku ya Jumatano watakutana na wamachinga, mama na baba lishe kwa ajili ya kuwekeana mikakati ya biashara.

 

Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema polisi imejipanga kuhakikisha abiria wote wanaosafiri au kuingia kituoni hapo hawapati usumbufu wa aina yoyote.

 

️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8​
️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment