×

Power Learn Project Yazinduliwa Nchini Kutoa Mafunzo ya Mifumo ya Kompyuta

Pichani kuanzia kushoto ni Mshirika wa ukuaji Power Learn Project (Bw. Hiroshi Yokoyama), Mkurugenzi wa Sahara Ventures (Bw. Jumanne Mtambalike), Mkurugenzi Mkuu wa Ukuaji wa Power Learn Project (Bi Mumbi Ndungu) na Muanzilishi mwenza wa Adanian Labs (Bw. Bendon Murgor)

 

 

Power Learn Project yazinduliwa Tanzania katika Hoteli ya Johari Rotana, Barabara ya Sokoine Drive, Dar es salaam, ikiwa inakusudia kushirikiana na serikali na wadau katika jitihada zake za kutoa mafunzo kwa wataalamu milioni 1 wa utengenezaji wa mifumo ya kompyuta (Software Developers) barani Afrika kufikia mwaka 2027.

 

Ubunifu kuelekea katika kufikia uchumi wa kidigitali wenye kujumuisha watu wote ni muhimu, unaendana sambamba na wakati kuhakikisha kwamba ubunifu unakuwa kiini cha mageuzi ya viwanda na utengenezaji wa ajira.

 

Power Learn Project (PLP) kwa kushirikiana na Adanian Labs Tanzania wamezindua program ya #1MillionDevs4Africa nchini Tanzania katika jitihada ya kutoa mafunzo kwa wataalamu wa utengenezaji wa mifumo ya kompyuta wapatao milioni 1 katika bara zima la Afrika kufikia mwaka 2027.  Tanzania ni nchi ya nne barani Africa, baada ya Kenya, Afrika Kusini na Zambia kutambulisha program ya #1Million Devs4 Africa.

 

Mwaka 2016, Tanzania ilizindua awamu ya pili ya mpango wa maendeleo ya miaka mitano (Five Year Development Plan (FYDP II) kwa dhumuni la kuongeza kasi kuelekea kufikia Mpango wa Maendeleo ya Tanzania kufikia mwaka 2025 (Tanzania Development Vision (TDV) 2025) – ambao ni mpango wa muda mrefu wa kubadilisha Tanzania kutoka katika kiwango kidogo cha tija na uzalishaji (low Productivity), uchumi wa kilimo na kufikia katika kutegemea maarifa na ufahamu, uchumi wa kati wa viwanda vidogo vidogo na vya kati kufikia mwaka 2025.

 

Teknolojia ya digitali ina nafasi kubwa sana katika kutatua vipengele vya Msingi vya malengo ya maendeleo. Jambo hili limewekewa msisitizo na Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ya mwaka 2016, ambayo inatoa msingi wa maendeleo na ukuaji wa sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Teknohama (ICT), kuiwezesha tasnia hiyo kuwakama kichocheo cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

 

Teknolojia ya kidigitali inaweza kusaidia kutatua aina mbalimbali za changamoto za kijamii na kiuchumi katika jamii. Hii ndio hali halisi katika nchi zinazoendelea ambako idadi kubwa ya watu haina uwezo wakufikia huduma za msingi, hasa kwa sababu ya kukosekana kwa rasilimali za kutosheleza na miundombinu hafifu.

 

Katika nchi nyingi, teknolojia ya internet inatumika kama mfumo wa kuboresha huduma za afya. elimu, biashara, usambazaji wa taarifa, ajira na ubunifu. “Kwa kutumia manufaa ya teknolojia ya simu za mkononi na digitali kusaidia kufikia malengo ya maendeleo nchini Tanzania, tunapaswa kushirikiana kwa karibu na wadau wote, ikiwemo serikali, taasisi za maendeleo, sekta binafsi, na tasnia ya simu za mkononi.

 

Kuna fursa ya kushirikiana zaidi miongoni mwa wadau wote kwa dhumuni la kukuza huduma za kidigitali kwa watu ambao hawajafikiwa na huduma hizo; kuwawezesha wanawake kimaendeleo na kupunguza aina zote za ukosefu wa usawa, kusaidia wataalamu chipukizi wa teknolojia.

 

Kiwango na matokeo ya ushirikiano katika kuboresha upatikanaji na upokeaji wa huduma za kidigitali unategemea na uwezo wa serikali kujenga mazingira yanayowezesha pamoja na motisha sahihi kwa washiriki.” Alisema Mumbi Ndung’u, Afisa Mkuu wa Ukuwaji na Uendeshaji, Power Learn Project.

 

PLP ni taasisiya kiafrika yenye nia ya kuleta mabadiliko yenye maono ya kuhamasisha mabadiliko kwa vijana Afrika kwa kuwapatia uwezo mahsusi wa kiteknolojia kupitia mafunzo bora ya teknolojia. Mradi wa PLP ulizinduliwa nchini Kenya mwezi Aprili, 2022.

 

PLP inakusudia kuanzisha taaluma katika mifumo ya kompyuta (Software) kwa kiwango cha awali, mafunzo yaliyokwisha lipiwa kwa kutumia upatikanaji wa data za bure na kujifunza kwa kuendana na kasi ya mwanafunzi kwa kipindi cha wiki 16.  Kozi zinazotolewa ni Pamoja na Programming Language, kama vile Python na Dart programming with Flutter to Blockchain 101, Database, Data Science na Ujuzi wa ujasiriamali.

 

Baada ya hapo wanafunzi watakuwa na fursa ya kufanya mazoezi kwa vitendo kupitia moduli za uthibitisho wa kazi. Wanafunzi watapata vyeti baada ya kukamilisha mafunzo na kujiunga na jamii ya Vijana wa Kiafrika wenye Ujuzi tayari kwaajili ya kuzifanyia kazi fursa za kidigitali.

 

Vile vile kupitia washirika wetu Afyarekod, wanafunzi watapatiwa ujuzi wa Maisha (life Skills) kama vile elimu ya fedha na afya ambao utawawezesha kupata msaada kwenye masuala ya afya ya akili. Ujuzi huu utawawezesha kukabiliana na mabadiliko ya kasi ya dunia kama wanajamii wazalishaji.

 

“Baada ya kukamilika kwa kozi, wanafunzi watakuwa na nafasi ya kupata fursa mbalimbali na elimu mbadala kupitia taasisi hiyo, ambayo ni pamoja na mafunzo kazini (internship) na fursa ya kupata uthibitisho wa kazi au kupata kituo cha mafunzo na kituo cha kuwaandaa na kuwaunganisha wataalamu hawa iwapo watakuwa wanataka kuangalia fursa za ujasiriamali”. Alieleza bi. Ndung’u.

 

Katika kipindi cha awali cha majaribio cha program nchini Tanzania, PLP inakusudia kuwapatia mafunzo watengenezaji wa mifumo ya kompyuta wapatao 1000 nchini Tanzania katika kipindi cha miezi minne.

 

Katika kipindi cha miezi michache inayofuata PLP inatazamia kuzindua nchi nyingi nne za majaribio ambazo ni Nigeria, Ghana, Uganda & Rwanda, ambapo Afrika magharibi na kaskazini zinatazamiwa kufuata katika awamu ya pili ya program hii. Udhamini wa mafunzo inapokea rasmi maombi tangu tarehe 19 Oktoba 2022.

 

“Dunia iko katika awamu ya nne ya mageuzi ya viwanda, ambayo inaendeshwa na Teknolojia ya Mawasiliano na Habari (ICT), kutokana na kwamba uchumi wa dunia na shughuli zingine zinategemea kwa kiasi kikubwa teknolojia ya mawasiliano na Habari (ICT). Kwa kuangalia hilo, Tanzania haiwezi kubakia nyuma” alisema Bwana John kamara, Mwenyekiti wa bodi ya Power Learn Project.

 

Kuhusu Power Learn Project:

Power Learn Project ni taasisi ya mabadiliko ambayo dhumuni lake ni kuleta mabadiliko kwa vijana Afrika kwa kuwawezesha kwa kuwapatia ujuzi stahiki kupitia utoaji wa mafunzo bora ya teknolojia.

Leave a Comment