
Moto wa gazeti la Ijumaa unazidi kutikisa kupitia Promosheni ya Chemshabongo yake ya msomaji wa gazeti hilo kujibu swali lililo katika ukurasa wa pili na kujishindia mkwanja wa Tsh 30,000.

Kama kawaida yake gazeti hilo kila linapotoka siku ya Ijumaa, Maofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa gazeti hilo, wameingia mtaani kuhamasisha na kutoa zawadi mbalimbali kwa wasomaji waliokutwa wakilisoma gazeti hil.

Miongoni mwa zawadi walizopewa ni pamoja na fulana kuwarudishia kiasi cha fedha wanayokuwa wamenunulia gazeti hilo.

Katika picha ni baadhi ya wasomaji wa gazeti hilo waliokabidhiwa zawadi wa maeneo ya Kawe jijini Dar es Saam na wengine waliokuwa wakielekezwa naomna ya kushirki chemshabongo hiyo.

Aidha, Ijumaa limesheheni kolamu zote kali zilizokuwa kwenye magazeti mengine Udaku ili kukufanya usi-miss kitu hata kimoja cha udaku iwe ndani ama nje ya Tanzania.



