×

Usiku wa Vitasa, Kinawaka Kesho Kinesi

WASWAHILI wanasema usiku wa deni hauchelewi kwisha, Usiku wa Vitasa uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni leo Jumamosi unahitimishwa kwenye Uwanja wa Kinesi Dar.

 

 

Fransic Miyayusho ‘Chichi Mawe’ na Habib Pengo ndiyo watu ambao wanasubiriwa kwa hamu kuonekana ulingoni hii leo katika pambano la raundi nane kg 61, kwa sababu hawa ndiyo wamebeba maana yenyewe ya pambano.

 

Jana Ijumaa mabondia zaidi ya 10 walipima uzito kwenye uwanja wa Kinesi huku tambo zikiwa zimetawala kila kona kwa mashabiki na mabondia wenyewe na Pengo akisema kama Chichi Mawe atafika raundi ya nane atavua gloves na kushuka ulingoni.

 

Mratibu wa pambano hilo kutoka Peak Time Media, Kapteni Seleman Semunyu aliliambia Championi kuwa: “Kila kitu kimekaa mahali pake na tunasubiri hiyo kesho watu waje kupata burudani ya ngumi kwa sababu hapa ndiyo tumefungua mwaka.”

 

Wakati Pengo na Miyayusho wakiwa ndiyo Main Card, Mfaume Mfaume atavaana na Yusuph Pembe, Haidari Mchanjo dhidi ya Mukhsini Swalehe ‘Alkasusu’, Waziri Rosta na Mwinyi Mzengela. Wengine ni Ismail Galiatano dhidi ya Baina Mazola, George Babucha na Hashim Zuberi.

 

 

Beka Ustadh dhidi ya Emmanuel Mwakyembe na Lukman Mohamed dhidi ya Mohamed Mpombo.

NA Issa Liponda

 

 

Leave a Comment