×

Shigongo Apendekeza Buchosa Ipandishwe Hadhi Kuwa Wilaya Kamili

 

MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo akiwa katika kikao Kamati Kuu ya Mkoa (RCC) ambapo amependekeza kupandishwa hadhi kwa halmashauri ya Buchosa kuwa wilaya kamili pamoja na Kisiwa cha Kome kuunda taarafa ya Kome.

 

Shigongo amesema Jimbo la Buchosa lina eneo kubwa sana, lina watu wengi na mapato yake ni makubwa, lakini wananchi wake wanakosa huduma muhimu kwa karibu na kulazimika kuzifuata Sengerema Mjini ama wakati mwingine Mwanza Mjini.

 

 

Hivyo amewaomba wajumbe wa mkutano huo mkuu wa mkoa waridhie Buchosa kuwa wilaya kamili na Kome kuwa taarafa ili kuwasogezea huduma hizo wananchi na kuharakisha maendeleo chanaya.

 

 

Aidha, Shigongo ameongeza kuwa wananchi wa Buchosa watafurahi sana kwani mara kwa mara walinamsumbua juu ya Buchosa kutangazwa kuwa wilaya kamili.

 

Wajumbe wa Kamati ya Mkoa wa Mwanza RCC wameridhia kwa pamoja kuwa Buchosa iwe wilaya kamili hivyo taratibu zingine za kiserikali zitafuata ikiwa ni pamoja na kuitangaza rasmi Buchosa kuwa wilaya kamili.

Leave a Comment