×

DC Ilala Atoa Siku 30 Bure Kufanya Biashara Soko la Minazi Mirefu

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija amefanya ziara katika Soko la Minazi Mirefu katika Ziara hiyo aliatambatana na Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe Omary Kumbilamoto pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaaam Wilaya ya Ilala Ndugu Jumanne Shauli.

 

 

Lengo la ziara hiyo kusikiliza changamoto za Wafanya biashara wadogo katika Soko hilo la Minazi Mirefu, Soko la Minazi Mirefu ni moja ya miradi mipya iliyojengwa na Manispaa ya Ilala kabla kuvunjwa kwake kuwa Jiji la Dar es salaam, Soko hilo kwa sasa limeanza kutoa huduma.

 

Mhe. Ludigija aliweza kupokea changamoto kutoka kwa wafanya biashara hao ikiwemo kuongezewa muda wa kulipa ushuru kwani hali ya kibiashara sio nzuri wateja bado hawajazoe soko hilo.

 

 

Aidha Mhe. Ludigija alizipokea changamoto zote na kutoa siku 30 kwa wafanya biashara hao kufanya biashara bure katika Soko hilo kwani lengo la Serikali kuwasaidia wananchi wanyonge.

 

Mhe. Ludigija aliendelea kwa kupiga marufuku watu kupangishana vizimba hivyo
“Serikali imejenga Soko hili ili mfanye biashara na sio mtu achukue kizimba alafu ampangishe mtu mwingine tukikubaini unafanya hivyo tunakuweka ndani” Alisema Mhe. Ludigija

 

 

Mwisho Mhe. Ludigija alimalizia kwa kuwataka wasimaizia wa Soko hilo kuahkikisha Soko hilo linawanufaisha wananchi wa Kata ya Minazi Mirefu.

Leave a Comment