×

Wawekezaji Wafurahia Soko la Bidhaa Tanzania

MKURUGENZI wa kampuni ya GF Vehicle Assemblers (GFA) Imran Kamali amefika kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kufanya kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Dk. Maduhu Kazi   yenye lengo la kujadili changamoto  mbali mbali na fursha za uwekezaji nchini Tanzania.

Kampuni ya GF inayomiliki kiwanda pekee cha kwanza nchini Tanzania kuunganisha magari ambacho kwa sasa wameanza na uunganishaji wa Maroli (Trucks) ambayo ndio ambayo yatampunguza gharama ya uagizaji magari hayo nje ya nchi hali itakayoweza kuimarisha na kupandisha bidhaa zetu kwa kutotumia fedha za kigeni katika kuagiza magari nje ya nchi

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha uwekezaji nchini  Dk. Kazi amewakaribisha wawekezaji kuiona fursa hiyo na kuichangamkia kwa kuanzisha miradi mingine kwenye eneo hilo kupitia TIC ili kunufaika na vivutio vya kiuwekezaji ambavyo Serikali imeboresha zaidi kwa ajili ya miradi ya aina hii nchini.

 

Mradi huu wa pekee na wa aina yake umesajiliwa TIC mwezi Februari 2020 na kuanza uzalishaji mwezi Septemba 2021 huko Kibaha, katika mradi huo watanzania takribani 100 wamepata ajira kwenye awamu ya kwanza ya utekelezaji na kiasi cha dola za Kimarekani milioni 2.5 kimewekezwa.

 

Aida mkurugenzi wa GF Imran Karmali amesema, anashukuru kwa ushirikiano alioupata na anaoendelea kuupata kutoka kwa viongozi mbali mbali wa serikali katika Kuhakikisha wanafanikiwa katika kufikika kufanikisha kuanza kwa mradi huo wa utengenezaji wa Magari

Pia alisema mpaka kukamilika kwa mradi huo kutaongeza soko la ajira kwa Watanzania katika Nyanja tofauti kuanzia mafundi na hata watoa huduma mbalimbali watahusika pia watahakikisha wanazalisha magari kwa soko la ndani nannje ya nchi pia hasa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Leave a Comment