
INJINIA wa Uholanzi, Lou Ottens, aliyesifika kwa kubuni kaseti ya sauti, amefariki akiwa na umri wa miaka 94. Inakadiriwa kuwa kaseti bilioni 100 zimeuzwa duniani tangu zilipobuniwa miaka ya 1960.
Uvumbuzi wa Ottens ulibadilisha jinsi watu walivyo sikiliza muziki, na katika miaka ya hivi karibuni kaseti zimeanza kutumika tena. Injinia huyo amefariki nyumbani kwake Duizel wikendi iliyopita, familia yake ilitangaza Jumanne wiki hii.

Ottens alikuwa mkuu wa kitengo cha utengenezaji bidhaa katika shirika la Philips miaka ya 1960, ambapo yeye na timu yake walitengeza kaseti.
Mwaka 1963, iliwasilishwa katika maonyesho ya bidhaa za kielektroniki ya Redio ya Berlin na muda mfupi baadae ikapata umaarufu duniani. Ottens pia ilihusika katika utengenezaji wa diski ndogo, na zaidi ya diski bilioni 200 ziliiuzwa duniani hadi leo.