
ALIYEKUWA Rais wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli aliongoza sala na madaktari pamoja na wahudumu wake hospitalini kabla ya kuaga dunia , kulingana na msemaji wa familia , Ngusa Samike, limeripoti gazeti la Citizen.

Msemaji wa familia amesema hayati Magufuli alipata sakramenti ya ‘mpako wa wagonjwa’ pamoja na dua akiwa pamoja na Askofu Mkuu wa zamani wa jimbo la Dar es salaam, Kadinali Polycarp Pengo, Padre wa Kanisa la St. Peter’s Alister Makubi, na Sheikh Mkuu wa Tanzania , Abubakar Zubeir.
Magufuli alifahamika kuwa na mahusiano ya karibu na viongozi wa kidini nchini Tanzania.