×

Majaliwa: Familia Imetutaka Mwili Ulale Tarehe 26 – Video

 

Serikali imetangaza mabadiliko ya utaratibu wa kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza katika viwanja vya Bunge Makao Makuu ya serikali ya nchi hiyo, Dodoma.

 

 

‘’Kutokana na uzoefu tuliopata Dar es Salaam kwa siku mbili, watu ni wengi mno, imebidi ratiba tuibadilishe kidogo, baada ya kuona matamanio ni makubwa.

 

“Utaratibu wa kuaga tumeubadilisha na hali ilivyokuwa Dar es Salaam, ili kila mmoja angalau aone jeneza, badala ya kwenda kuaga kwa kumuangalia.

 

“Tutakachofanya ni kuzungusha mwili mara tatu uwanja, kisha tutazungusha mwili mtaani, tumeshuhudia watoto wadogo, wazee, hatutamudu, maana familia imetutaka mwili huu ulale tarehe 26, kesho tutakua Zanzibar, kesho kutwa Mwanza,” amesema Majaliwa.

 

Leave a Comment